10. Mwenyezi-Mungu amewamiminia hali ya usingizi mzito;ameyafumba macho yenu enyi manabii,amefunika vichwa vyenu enyi waonaji.
11. Basi, kwenu nyinyi maono yote haya ni kama ujumbe ulioandikwa katika kitabu kilichofungwa kwa mhuri. Ukimpelekea mtu yeyote ajuaye kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atasema, “Siwezi kukisoma kwani kimefungwa kwa mhuri.”
12. Na ukimpa mtu yeyote asiyejua kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atakuambia, “Sijui kusoma.”
13. Bwana asema,“Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu,hali mioyo yao iko mbali nami.Wananiheshimu kulingana na mapokeo ya watu tu,jambo walilojifunza wao wenyewe.
14. Hivyo, nitawatenda tena watu hawa maajabu,mambo ya ajabu na ya kushangaza.Nao wenye hekima wao wataishiwa hekima,na busara ya wenye busara wao itatoweka.
15. “Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu,mnaotenda matendo yenu gizanina kusema: ‘Hamna atakayetuona;nani awezaye kujua tunachofanya?’