4. Mtumaini Mwenyezi-Mungu siku zotekwa maana yeye ni mwamba wa usalama milele.
5. Amewaporomosha waliokaa pande za juu,mji maarufu ameuangusha mpaka chini,ameutupa mpaka mavumbini.
6. Sasa mji huo unakanyagwakanyagwakwa miguu ya watu maskini na fukara.
7. Njia ya watu wanyofu ni rahisi;ewe Mungu mwadilifu, wasawazisha njia yao.
8. Katika njia ya maamuzi yakotunakungojea ee Mwenyezi-Mungu;kulikumbuka jina lako ndiyo tamaa yetu.
9. Moyo wangu wakutamani usiku kucha,nafsi yangu yakutafuta kwa moyo.Utakapoihukumu dunia,watu wote ulimwenguni watajifunza haki.
10. Lakini waovu hata wakipewa fadhili,hawawezi kujifunza kutenda haki.Hata katika nchi ya wanyofu,wao bado wanatenda maovu,wala hawajali ukuu wako wewe Mwenyezi-Mungu.
11. Ee Mwenyezi-Mungu umeinua mkono kuwaadhibu,lakini maadui zako hawauoni.Waoneshe uwapendavyo watu wako nao wataaibika.Moto wa hasira yako uwateketeze maadui zako!
12. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, umetupatia amani;umefanikisha shughuli zetu zote.
13. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,tulipata kutawaliwa na watu wengine na miungu yao,lakini twakiri wewe pekee kuwa Mungu wetu.
14. Watu hao wamekufa, wala hawataishi tena;wamekuwa mizimu, wala hawatafufuka.Maana wewe umewaadhibu na kuwaangamiza,hakuna atakayeweza kuwakumbuka tena.