22. Vilevile mtatoa beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
23. “Siku ya nne mtatoa: Fahali kumi, kondoo madume wawili, wanakondoo kumi na wanne, wasio na dosari.
24. Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali na kondoo na wanakondoo kulingana na idadi yao, kama inavyotakiwa.
25. Mtatoa pia beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi licha ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
26. “Siku ya tano, mtatoa fahali tisa, kondoo wawili, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na dosari.
27. Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali na kondoo na wanakondoo kulingana na idadi yao kama inavyotakiwa.
28. Mtatoa pia beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
29. “Siku ya sita mtatoa fahali wanane, kondoo madume wawili, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na dosari.
30. Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali, kondoo dume na wanakondoo kulingana na idadi yao, kama inavyotakiwa.
31. Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji.
32. “Siku ya saba mtatoa fahali saba, kondoo madume watatu, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja, wasio na dosari.
33. Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali, kondoo dume, na wanakondoo, kulingana na idadi yao, kama wanavyotakiwa.
34. Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.