Habakuki 3:16-19 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Nasikia hayo nami ninashtuka mwilini,midomo yangu inatetemeka kwa hofu;mifupa yangu inateguka,miguu yangu inatetemeka.Ninangojea kwa utulivu siku ile ya maafa,ambayo inawajia wale wanaotushambulia.

17. Hata kama mitini isipochanua maua,wala mizabibu kuzaa zabibu;hata kama mizeituni isipozaa zeituni,na mashamba yasipotoa chakula;hata kama kondoo wakitoweka zizini,na mifugo kukosekana mazizini,

18. mimi nitaendelea kumfurahia Mwenyezi-Mungunitamshangilia Mungu anayeniokoa.

19. Bwana, Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu,huiimarisha miguu yangu kama ya paa,huniwezesha kupita juu milimani.

Habakuki 3