14. Tarumbeta imepigwa na kuwafanya wote wawe tayari.Lakini hakuna anayekwenda vitani,kwani ghadhabu yangu iko juu ya umati wote.
15. Nje kuna kifo kwa upangana ndani ya mji kuna maradhi mabaya na njaa.Walioko shambani watakufa kwa upanga;walio mjini njaa na maradhi mabaya yatawaangamiza.
16. Wakiwapo watu watakaosalimikawatakimbilia milimani kama hua waliotishwa bondeni.Kila mmoja wao ataomboleza kwa dhambi zake.
17. Kila mtu, mikono yake itakuwa dhaifuna magoti yake yatakuwa maji.
18. Watavaa mavazi ya gunia,hofu itawashika,nao watakuwa na aibu,vichwa vyao vyote vitanyolewa.
19. Watatupa fedha yao barabaranina dhahabu yao itakuwa kama kitu najisi.Fedha na dhahabu zao hazitaweza kuwaokoakatika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu;wala hawataweza kushibaau kuyajaza matumbo yao fedha na dhahabu waliyojirundikia;kwani mali hiyo ndiyo chanzo cha dhambi yao.