Ezekieli 41:2-8 Biblia Habari Njema (BHN)

2. na upana wa mita 5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita 2.5. Akaupima ukumbi wenyewe, nao ulikuwa na urefu wa mita 20 na upana mita 10.

3. Kisha akaenda kwenye chumba cha ndani kabisa. Akaipima nafasi iliyoelekea huko, nayo ilikuwa na kimo cha mita 1 na upana mita 3.5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita tatu u nusu.

4. Akakipima chumba chenyewe, nacho kilikuwa cha mraba pande zake zikiwa na upana wa mita 10. Chumba hiki kilikuwa mbele ya ukumbi wa katikati. Kisha, akaniambia, “Hapa ndipo mahali patakatifu kabisa.”

5. Yule mtu aliupima unene wa ukuta wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nao ulikuwa mita tatu. Kulikuwa na mfululizo wa vyumba vidogovidogo kuizunguka nyumba ya Mwenyezi-Mungu, vyenye upana wa mita mbili.

6. Vyumba hivi, vilikuwa katika majengo ya ghorofa tatu, na kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Ukuta wa nje wa hekalu kila kwenye ghorofa ulikuwa mwembamba kuliko ule wa ghorofa ya chini, ili vile vyumba viwe imara bila ya kuutegemea ukuta wa hekalu.

7. Kwa upande, zile kuta za hekalu zikitazamwa kutokea nje, zilionekana kuwa na unene uleule toka chini hadi juu. Mkabala na ukuta wa nje wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nje ya vyumba, kulikuwa na ngazi mbili, ambazo zilifanya iwe rahisi kwenda juu kutokea ghorofa ya chini hadi ile ya juu.

8. Kisha, nikaona kuwa hekalu lilikuwa na sakafu iliyonyanyuliwa kulizunguka, nayo ilikuwa ndio msingi wa zile ghorofa tatu mkabala na hekalu, kimo cha msingi wa ghorofa hizo ulikuwa sawa na ule ufito wa kupimia, mita tatu.

Ezekieli 41