14. Urefu mbele ya hekalu tangu upande huu hadi upande huu ukichanganya na ile nafasi wazi, ulikuwa pia mita 50.
15. Yule mtu akapima urefu wa jengo hadi magharibi pamoja na mabaraza yake pande zake zote, nalo lilikuwa na urefu wa mita 50.Chumba cha kuingilia hekaluni, mahali patakatifu, na mahali patakatifu kabisa,
16. vyote vilipambwa kwa mbao tangu sakafuni hadi kwenye madirisha. Madirisha haya yangeweza kufunikwa.
17. Mpaka kwenye nafasi juu ya mlango hata kwenye chumba cha ndani na nje yake, pia juu ya kuta ndani ya chumba cha ndani na kwenye ukumbi palikuwapo na michoro iliyofanana na
18. mitende na picha za viumbe wenye mabawa. Kila baada ya mtende kulichorwa picha ya kiumbe chenye mabawa kukizunguka chumba chote. Kila kiumbe alikuwa na nyuso mbili:
19. Uso wa mwanadamu ulioelekea kwenye mtende upande mmoja na uso wa simba ulioelekea kwenye mtende wa upande mwingine. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwenye nyumba nzima,
20. tangu sakafu hadi juu ya milango palichorwa viumbe wenye mabawa na mitende.
21. Miimo ya mahali patakatifu ilikuwa ya mraba.Mbele ya mlango wa kuingilia mahali patakatifu kabisa kulikuwa na kitu kilichoonekana kama
22. madhabahu ya mbao. Kimo chake kilikuwa nusu mita na upana wa mita moja. Pembe zake, tako lake, na pande zake zote zilikuwa zimetengenezwa kwa mbao. Yule mtu akaniambia, “Hii ndiyo meza inayokaa mbele ya Mwenyezi-Mungu.”
23. Kulikuwako na mlango wa tarabe wa kuingia kwenye ukumbi wa hekalu na mlango wa tarabe wa kuingia mahali patakatifu kabisa.
24. Milango hiyo ilikuwa ya tarabe, kwa hiyo kila mlango uliweza kufunguka katikati.
25. Kwenye mlango wa kuingilia ukumbi kulichorwa viumbe vyenye mabawa na mitende, kama ilivyokuwa kwenye kuta. Na kulikuwa na kifuniko cha ubao kikifunika mlango kwa nje kwenye sehemu ya kuingilia ndani.
26. Pembeni mwa chumba hiki, kulikuwa na madirisha madogo na kuta zilipambwa kwa michoro ya mitende.