Ezekieli 41:14-21 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Urefu mbele ya hekalu tangu upande huu hadi upande huu ukichanganya na ile nafasi wazi, ulikuwa pia mita 50.

15. Yule mtu akapima urefu wa jengo hadi magharibi pamoja na mabaraza yake pande zake zote, nalo lilikuwa na urefu wa mita 50.Chumba cha kuingilia hekaluni, mahali patakatifu, na mahali patakatifu kabisa,

16. vyote vilipambwa kwa mbao tangu sakafuni hadi kwenye madirisha. Madirisha haya yangeweza kufunikwa.

17. Mpaka kwenye nafasi juu ya mlango hata kwenye chumba cha ndani na nje yake, pia juu ya kuta ndani ya chumba cha ndani na kwenye ukumbi palikuwapo na michoro iliyofanana na

18. mitende na picha za viumbe wenye mabawa. Kila baada ya mtende kulichorwa picha ya kiumbe chenye mabawa kukizunguka chumba chote. Kila kiumbe alikuwa na nyuso mbili:

19. Uso wa mwanadamu ulioelekea kwenye mtende upande mmoja na uso wa simba ulioelekea kwenye mtende wa upande mwingine. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwenye nyumba nzima,

20. tangu sakafu hadi juu ya milango palichorwa viumbe wenye mabawa na mitende.

21. Miimo ya mahali patakatifu ilikuwa ya mraba.Mbele ya mlango wa kuingilia mahali patakatifu kabisa kulikuwa na kitu kilichoonekana kama

Ezekieli 41