1. Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Wewe mtu! Toa unabii kuhusu milima ya Israeli. Iambie isikilize maneno yangu
2. mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Maadui zenu wamewazomea na kusema kuwa nyinyi mmekuwa mali yao!
3. “Kwa hiyo, wewe Ezekieli, toa unabii useme kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Watu wamewafanya nyinyi milima ya Israeli kuwa tupu na kuwavamia kutoka kila upande hata mmekuwa mali ya mataifa mengine, mkawa kitu cha kusimangwa na kudhihakiwa miongoni mwa watu!
4. Kwa hiyo, enyi milima ya Israeli, sikieni neno langu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu: Nyinyi milima na vilima, mifereji na mabonde, nyika tupu na miji mmehamwa, mkatekwa nyara na kudharauliwa na mataifa yote yanayowazungukeni.
5. Sasa kwa kuwa mimi nimechukizwa mno, nitayaadhibu mataifa mengine na hasa watu wa Edomu. Wao kwa furaha moyoni na madharau waliichukua hiyo nchi iliyo yangu iwe yao.