3. Haya! Wewe wajiona mwenye hekima kuliko Danieli,wadhani hakuna siri yoyote usiyoijua.
4. Kwa hekima na akili yakoumejipatia utajiri,umejikusanyia dhahabu na fedhaukaziweka katika hazina zako.
5. Kwa busara yako kubwa katika biasharaumejiongezea utajiri wako,ukawa na kiburi kwa mali zako!
6. Kwa hiyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Kwa vile unajiona mwenye hekima kama Mungu,
7. basi nitakuletea watu wageni,mataifa katili kuliko yote.Wataharibu fahari ya hekima yakona kuchafua uzuri wako.
8. Watakutumbukiza chini shimoni,nawe utakufa kifo cha kikatili kilindini mwa bahari.
9. Je, utajiona bado kuwa mungumbele ya hao watakaokuua?Mikononi mwa hao watakaokuangamiza,utatambua kuwa wewe ni mtu tu, wala si Mungu!
10. Utakufa kifo cha aibu kubwamikononi mwa watu wa mataifa.Ni mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”
11. Tena neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
12. “Wewe mtu! Imba wimbo wa maombolezo juu ya mfalme wa Tiro. Mwambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Wewe mfalme wa Tiro ulikuwa upeo wa ukamilifu;ulijaa hekima na uzuri kamili.
13. Ulikaa Edeni, bustani ya Mungu.Ulipambwa kwa kila namna ya johari,akiki, topazi, yaspi, zabarajadi, berili,sardoniki, johari ya rangi ya samawati, almasi na zumaridi.Ulikuwa na mapambo ya dhahabu.Yote uliwekewa tayari siku ulipoumbwa.
14. Nilimteua malaika kukulinda,uliishi katika mlima wangu mtakatifuna kutembea juu ya vito vinavyometameta.
15. Uliishi maisha yasiyo na lawama,tangu siku ile ulipoumbwa,hadi ulipoanza kufanya uovu.
16. Ufanisi wa biashara yakoulikujaza dhuluma, ukatenda dhambi.Kwa hiyo nilikufukuza kama kinyaa,mbali na mlima wangu mtakatifu.Na yule malaika aliyekulindaakakufukuzia mbali na vito vinavyometameta.