Zek. 6:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, yanatokea magari ya vita manne, yanatoka kati ya milima miwili, na milima hiyo ilikuwa ni milima ya shaba.

2. Katika gari la kwanza walikuwa farasi wekundu; na katika gari la pili walikuwa farasi weusi;

3. na katika gari la tatu walikuwa farasi weupe; na katika gari la nne walikuwa farasi wa rangi ya kijivujivu.

4. Nikajibu, nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Hawa ni nini, Bwana wangu?

5. Malaika akajibu, akaniambia, Hawa ni pepo nne za mbinguni, zitokeazo baada ya kusimama mbele za Bwana wa dunia yote.

Zek. 6