1. Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.
2. BWANA akamwambia Shetani, BWANA na akukemee Ewe Shetani; naam, BWANA, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?
3. Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.
4. Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi.