Zek. 11:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Ifungue milango yako, Ee Lebanoni,Ili moto uiteketeze mierezi yako.

2. Piga yowe, msunobari, maana mwerezi umeanguka,Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika;Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani,Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.

3. Sauti ya wachungaji, ya uchungu mwingi!Kwa maana utukufu wao umeharibika;Sauti ya ngurumo ya wana-simba!Kwa maana kiburi cha Yordani kimeharibika.

4. BWANA, Mungu wangu, alisema hivi, Lilishe kundi la machinjo,

5. ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe BWANA, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.

6. Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema BWANA; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa mikononi mwao.

Zek. 11