Zab. 99:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka;Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.

2. BWANA katika Sayuni ni mkuu,Naye ametukuka juu ya mataifa yote.

3. Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa;Ndiye mtakatifu.

Zab. 99