Zab. 98:4-8 Swahili Union Version (SUV)

4. Mshangilieni BWANA, nchi yote,Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.

5. Mwimbieni BWANA zaburi kwa kinubi,Kwa kinubi na sauti ya zaburi.

6. Kwa panda na sauti ya baragumu.Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA.

7. Bahari na ivume na vyote viijazavyo,Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.

8. Mito na ipige makofi,Milima na iimbe pamoja kwa furaha.

Zab. 98