Zab. 96:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Mwimbieni BWANA, nchi yote.

2. Mwimbieni BWANA, libarikini jina lake,Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.

3. Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,Na watu wote habari za maajabu yake.

4. Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana.Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.

5. Maana miungu yote ya watu si kitu,Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.

Zab. 96