Zab. 96:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Mwimbieni BWANA, nchi yote.

2. Mwimbieni BWANA, libarikini jina lake,Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.

3. Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,Na watu wote habari za maajabu yake.

Zab. 96