12. Ee BWANA, heri mtu yule umwadibuye,Na kumfundisha kwa sheria yako;
13. Upate kumstarehesha siku za mabaya,Hata asiye haki atakapochimbiwa shimo.
14. Kwa kuwa BWANA hatawatupa watu wake,Wala hutauacha urithi wake,
15. Maana hukumu itairejea haki,Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.
16. Ni nani atakayesimamaKwa ajili yangu juu ya wabaya?Ni nani atakayenisaidiaJuu yao wafanyao maovu?
17. Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu,Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.
18. Niliposema, Mguu wangu unateleza;Ee BWANA, fadhili zako zilinitegemeza.
19. Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu,Faraja zako zaifurahisha roho yangu.
20. Je! Kiti cha udhalimu kishirikiane nawe,Kitungacho madhara kwa njia ya sheria?
21. Huishambulia nafsi yake mwenye haki,Na kuihukumu damu isiyo na hatia.
22. Lakini BWANA amekuwa ngome kwangu,Na Mungu wangu mwamba wangu wa kukimbilia.