8. Ila kwa macho yako utatazama,Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9. Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.
10. Mabaya hayatakupata wewe,Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11. Kwa kuwa atakuagizia malaika zakeWakulinde katika njia zako zote.
12. Mikononi mwao watakuchukua,Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.