11. Kwa kuwa atakuagizia malaika zakeWakulinde katika njia zako zote.
12. Mikononi mwao watakuchukua,Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13. Utawakanyaga simba na nyoka,Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
14. Kwa kuwa amekaza kunipendaNitamwokoa; na kumweka palipo juu,Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15. Ataniita nami nitamwitikia;Nitakuwa pamoja naye taabuni,Nitamwokoa na kumtukuza;