1. Aketiye mahali pa siri pake Aliye juuAtakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2. Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,Mungu wangu nitakayemtumaini.
3. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,Na katika tauni iharibuyo.
4. Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5. Hutaogopa hofu ya usiku,Wala mshale urukao mchana,
6. Wala tauni ipitayo gizani,Wala uele uharibuo adhuhuri,