Zab. 9:11-19 Swahili Union Version (SUV)

11. Mwimbieni BWANA akaaye Sayuni,Yatangazeni kati ya watu matendo yake.

12. Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka,Hakukisahau kilio cha wanyonge.

13. Wewe, BWANA, unifadhili,Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia;Wewe uniinuaye katika malango ya mauti,

14. Ili nizisimulie sifa zako zote;Katika malango ya binti SayuniNitaufurahia wokovu wako.

15. Mataifa wamezama katika shimo walilolifanya;Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao.

16. BWANA amejidhihirisha na kutekeleza hukumu;Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.

17. Wadhalimu watarejea kuzimu,Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.

18. Kwa maana mhitaji hatasahauliwa daima;Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.

19. BWANA, usimame, mwanadamu asipate nguvu,Mataifa wahukumiwe mbele zako.

Zab. 9