Zab. 9:10-16 Swahili Union Version (SUV)

10. Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe,Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.

11. Mwimbieni BWANA akaaye Sayuni,Yatangazeni kati ya watu matendo yake.

12. Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka,Hakukisahau kilio cha wanyonge.

13. Wewe, BWANA, unifadhili,Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia;Wewe uniinuaye katika malango ya mauti,

14. Ili nizisimulie sifa zako zote;Katika malango ya binti SayuniNitaufurahia wokovu wako.

15. Mataifa wamezama katika shimo walilolifanya;Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao.

16. BWANA amejidhihirisha na kutekeleza hukumu;Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.

Zab. 9