Zab. 9:1-12 Swahili Union Version (SUV)

1. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote;Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;

2. Nitafurahi na kukushangilia Wewe;Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu.

3. Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma;Hujikwaa na kuangamia mbele zako.

4. Kwa maana umenifanyia hukumu na hakiUmeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki.

5. Umewakemea mataifa;Na kumwangamiza mdhalimu;Umelifuta jina lao milele na milele;

6. Adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele.Nayo miji yao uliing’oa;Hata kumbukumbu lao limepotea.

7. Bali BWANA atakaa milele,Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu.

8. Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki;Atawaamua watu kwa adili.

9. BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa,Naam, ngome kwa nyakati za shida.

10. Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe,Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.

11. Mwimbieni BWANA akaaye Sayuni,Yatangazeni kati ya watu matendo yake.

12. Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka,Hakukisahau kilio cha wanyonge.

Zab. 9