6. Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na BWANA?Ni nani afananaye na BWANA miongoni mwa malaika?
7. Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu,Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
8. BWANA, Mungu wa majeshi,Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee YAHU?Na uaminifu wako unakuzunguka.
9. Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi cha bahari.Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe.
10. Ndiwe uliyemseta Rahabu akawa kama aliyeuawa,Kwa mkono hodari umewatawanya wakuchukiao.
11. Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako,Ulimwengu na vyote viujazavyoNdiwe uliyeupiga msingi wake.
12. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba,Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.