Zab. 89:5-16 Swahili Union Version (SUV)

5. Ee BWANA, mbingu zitayasifu maajabu yako,Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.

6. Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na BWANA?Ni nani afananaye na BWANA miongoni mwa malaika?

7. Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu,Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

8. BWANA, Mungu wa majeshi,Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee YAHU?Na uaminifu wako unakuzunguka.

9. Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi cha bahari.Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe.

10. Ndiwe uliyemseta Rahabu akawa kama aliyeuawa,Kwa mkono hodari umewatawanya wakuchukiao.

11. Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako,Ulimwengu na vyote viujazavyoNdiwe uliyeupiga msingi wake.

12. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba,Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.

13. Mkono wako ni mkono wenye uweza,Mkono wako una nguvu,Mkono wako wa kuume umetukuka.

14. Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako,Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.

15. Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe,Ee BWANA, huenenda katika nuru ya uso wako.

16. Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa,Na kwa haki yako hutukuzwa.

Zab. 89