Zab. 89:40-47 Swahili Union Version (SUV)

40. Umeyabomoa maboma yake yote,Umezifanya ngome zake kuwa magofu.

41. Wote wapitao njiani wanateka mali zake;Amekuwa laumu kwa jirani zake;

42. Umeutukuza mkono wa kuume wa watesi wake;Umewafurahisha wote wanaomchukia.

43. Pia umeurudisha nyuma ukali wa upanga wake;Wala hukumsimamisha vitani.

44. Umeikomesha fahari yake;Kiti chake cha enzi umekitupa chini.

45. Umezipunguza siku za ujana wake;Umemvika aibu.

46. Ee BWANA, hata lini? Utajificha hata milele?Ghadhabu yako itawaka kama moto?

47. Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wa kudumu;Kwa ubatili gani umeiumba jamii ya wanadamu!

Zab. 89