Zab. 89:2-14 Swahili Union Version (SUV)

2. Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.

3. Nimefanya agano na mteule wangu,Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu.

4. Wazao wako nitawafanya imara milele,Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.

5. Ee BWANA, mbingu zitayasifu maajabu yako,Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.

6. Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na BWANA?Ni nani afananaye na BWANA miongoni mwa malaika?

7. Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu,Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

8. BWANA, Mungu wa majeshi,Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee YAHU?Na uaminifu wako unakuzunguka.

9. Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi cha bahari.Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe.

10. Ndiwe uliyemseta Rahabu akawa kama aliyeuawa,Kwa mkono hodari umewatawanya wakuchukiao.

11. Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako,Ulimwengu na vyote viujazavyoNdiwe uliyeupiga msingi wake.

12. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba,Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.

13. Mkono wako ni mkono wenye uweza,Mkono wako una nguvu,Mkono wako wa kuume umetukuka.

14. Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako,Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.

Zab. 89