1. Fadhili za BWANA nitaziimba milele;Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
2. Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.
3. Nimefanya agano na mteule wangu,Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu.
4. Wazao wako nitawafanya imara milele,Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.