5. Miongoni mwao waliokufa nimetupwa,Kama waliouawa walalao makaburini.Hao ambao Wewe huwakumbuki tena,Wametengwa mbali na mkono wako.
6. Mimi umenilaza katika shimo la chini,Katika mahali penye giza vilindini.
7. Ghadhabu yako imenilemea,Umenitesa kwa mawimbi yako yote.
8. Wanijuao umewatenga nami;Umenifanya kuwa chukizo kwao;Nimefungwa wala siwezi kutoka.
9. Jicho langu limefifia kwa ajili ya matesoBWANA, nimekuita kila siku;Nimekunyoshea Wewe mikono yangu.
10. Wafu je! Utawafanyia miujiza?Au waliofariki watasimama na kukuhimidi?
11. Fadhili zako zitasimuliwa kaburini?Au uaminifu wako katika uharibifu?