11. Fadhili zako zitasimuliwa kaburini?Au uaminifu wako katika uharibifu?
12. Miujiza yako itajulikana gizani?Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?
13. Lakini mimi nimekulilia Wewe, BWANA,Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.
14. BWANA, kwa nini kuitupa nafsi yangu,Na kunificha uso wako?
15. Nateswa mimi hali ya kufa tangu ujana,Nimevumilia vitisho vyako na kufadhaika.
16. Hasira zako kali zimepita juu yangu,Maogofyo yako yameniangamiza.
17. Yamenizunguka kama maji mchana kutwa,Yamenisonga yote pamoja.