Zab. 86:5-14 Swahili Union Version (SUV)

5. Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema,Umekuwa tayari kusamehe,Na mwingi wa fadhili,Kwa watu wote wakuitao.

6. Ee BWANA, uyasikie maombi yangu;Uisikilize sauti ya dua zangu.

7. Siku ya mateso yangu nitakuita,Kwa maana utaniitikia.

8. Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana,Wala matendo mfano wa matendo yako.

9. Mataifa yote uliowafanya watakuja;Watakusujudia Wewe, Bwana,Watalitukuza jina lako;

10. Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu,Wewe ndiwe mfanya miujiza,Ndiwe Mungu peke yako.

11. Ee BWANA, unifundishe njia yako;Nitakwenda katika kweli yako;Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;

12. Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu,Kwa moyo wangu wote,Nitalitukuza jina lako milele.

13. Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana;Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.

14. Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia;Mkutano wa wakatili wamenitafuta roho.Wala hawakukuweka WeweMbele ya macho yao.

Zab. 86