1. Ee BWANA, utege sikio lako unijibu,Maana mimi ni maskini na mhitaji
2. Unihifadhi nafsi yangu,Maana mimi ni mcha Mungu.Wewe uliye Mungu wangu,Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini.
3. Wewe, Bwana, unifadhili,Maana nakulilia Wewe mchana kutwa.
4. Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako,Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.
5. Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema,Umekuwa tayari kusamehe,Na mwingi wa fadhili,Kwa watu wote wakuitao.
6. Ee BWANA, uyasikie maombi yangu;Uisikilize sauti ya dua zangu.
7. Siku ya mateso yangu nitakuita,Kwa maana utaniitikia.
8. Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana,Wala matendo mfano wa matendo yako.