1. BWANA, umeiridhia nchi yako,Umewarejeza mateka wa Yakobo.
2. Umeusamehe uovu wa watu wako,Umezisitiri hatia zao zote.
3. Umeiondoa ghadhabu yako yote,Umerudi na kuuacha ukali wa hasira yako.
4. Mungu wa wokovu wetu, uturudishe,Uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.
5. Je! Utatufanyia hasira hata milele?Utadumisha ghadhabu kizazi hata kizazi?
6. Je! Hutaki kurudi na kutuhuisha,Watu wako wakufurahie?
7. Ee BWANA, utuonyeshe rehema zako,Utupe wokovu wako.