Zab. 83:4-8 Swahili Union Version (SUV)

4. Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa,Na jina la Israeli halitakumbukwa tena.

5. Maana wanashauriana kwa moyo mmoja,Juu yako wanafanyana agano.

6. Hema za Edomu, na Waishmaeli,Na Moabu, na Wahagari,

7. Gebali, na Amoni, na Amaleki,Na Filisti, nao wanaokaa Tiro,

8. Ashuri naye amepatana nao,Wamewasaidia wana wa Lutu.

Zab. 83