7. Katika shida uliniita nikakuokoa;Nalikuitikia katika sitara ya radi;Nalikujaribu penye maji ya Meriba.
8. Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya,Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza;
9. Usiwe na mungu mgeni ndani yako;Wala usimsujudie mungu mwingine.
10. Mimi ndimi BWANA, Mungu wako,Niliyekupandisha toka nchi ya Misri;Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.
11. Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu,Wala Israeli hawakunitaka.
12. Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao,Waenende katika mashauri yao.
13. Laiti watu wangu wangenisikiliza,Na Israeli angeenenda katika njia zangu;
14. Ningewadhili adui zao kwa upesi,Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu;
15. Wamchukiao BWANA wangenyenyekea mbele zake,Bali wakati wao ungedumu milele.