1. Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha,Mshangilieni Mungu wa Yakobo.
2. Pazeni zaburi, pigeni matari,Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.
3. Pigeni panda mwandamo wa mwezi,Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.
4. Kwa maana ni sheria kwa Israeli,Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo.
5. Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu,Alipoondoka juu ya nchi ya Misri;Maneno yake nisiyemjua naliyasikia.
6. Nimelitenga bega lake na mzigo,Mikono yake ikaachana na kikapu.
7. Katika shida uliniita nikakuokoa;Nalikuitikia katika sitara ya radi;Nalikujaribu penye maji ya Meriba.