11. Nao uliyaeneza matawi yake hata baharini,Na vichipukizi vyake hata kunako Mto.
12. Kwa nini umezibomoa kuta zake,Wakauchuma wote wapitao njiani?
13. Nguruwe wa msituni wanauharibu,Na hayawani wa kondeni wanautafuna.
14. Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi,Utazame toka juu uone, uujilie mzabibu huu.
15. Na mche ule ulioupandaKwa mkono wako wa kuume;Na tawi lile ulilolifanyaKuwa imara kwa nafsi yako.
16. Umechomwa moto; umekatwa;Kwa lawama ya uso wako wanapotea.