Zab. 76:2-9 Swahili Union Version (SUV)

2. Kibanda chake pia kiko Salemu,Na maskani yake iko Sayuni.

3. Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta,Ngao, na upanga, na zana za vita.

4. Wewe U mwenye fahari na adhama,Toka milima ya mateka.

5. Wametekwa wenye moyo thabiti;Wamelala usingizi;Wala hawakuiona mikono yaoWatu wote walio hodari.

6. Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.

7. Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe;Naye ni nani awezaye kusimama ufanyapo hasira?

8. Toka mbinguni ulitangaza hukumu;Nchi iliogopa, ikakaa kimya.

9. Mungu aliposimama ili kuhukumuNa kuwaokoa wapole wa dunia wote pia.

Zab. 76