1. Katika Yuda Mungu amejulikana,Katika Israeli jina lake ni kuu.
2. Kibanda chake pia kiko Salemu,Na maskani yake iko Sayuni.
3. Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta,Ngao, na upanga, na zana za vita.
4. Wewe U mwenye fahari na adhama,Toka milima ya mateka.
5. Wametekwa wenye moyo thabiti;Wamelala usingizi;Wala hawakuiona mikono yaoWatu wote walio hodari.
6. Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.