2. Ulikumbuke kusanyiko lako,Ulilolinunua zamani.Ulilolikomboa liwe kabila ya urithi wako,Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.
3. Upainulie miguu yako palipoharibika milele;Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.
4. Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako;Wameweka bendera zao ziwe alama.
5. Wanaonekana kama watu wainuao mashoka,Waikate miti ya msituni.
6. Na sasa nakishi yake yote piaWanaivunja-vunja kwa mashoka na nyundo.
7. Wamepatia moto patakatifu pako;Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.
8. Walisema mioyoni mwao,Na tuwaangamize kabisa;Mahali penye mikutano ya MunguWamepachoma moto katika nchi pia.