Zab. 74:14-22 Swahili Union Version (SUV)

14. Wewe uliviseta vichwa vya lewiathani,Awe chakula cha watu wa jangwani.

15. Wewe ulitokeza chemchemi na kijito;Wewe ulikausha mito yenye maji sikuzote.

16. Mchana ni wako, usiku nao ni wako,Ndiwe uliyeufanya mwanga na jua.

17. Wewe uliiweka mipaka yote ya dunia,Kaskazi na kusi Wewe ulizitengeneza.

18. Ee BWANA, uyakumbuke hayo, adui amelaumu,Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.

19. Usimpe mnyama mkali nafsi ya hua wako;Usiusahau milele uhai wa watu wako walioonewa.

20. Ulitafakari agano;Maana mahali penye giza katika nchiPamejaa makao ya ukatili.

21. Aliyeonewa asirejee ametiwa haya,Mnyonge na mhitaji na walisifu jina lako.

22. Ee Mungu, usimame, ujitetee mwenyewe,Ukumbuke unavyotukanwa na mpumbavu mchana kutwa.

Zab. 74