1. Ee Mungu, mbona umetutupa milele?Kwa nini hasira yako inatoka moshiJuu ya kondoo wa malisho yako?
2. Ulikumbuke kusanyiko lako,Ulilolinunua zamani.Ulilolikomboa liwe kabila ya urithi wako,Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.
3. Upainulie miguu yako palipoharibika milele;Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.
4. Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako;Wameweka bendera zao ziwe alama.
5. Wanaonekana kama watu wainuao mashoka,Waikate miti ya msituni.
6. Na sasa nakishi yake yote piaWanaivunja-vunja kwa mashoka na nyundo.
7. Wamepatia moto patakatifu pako;Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.
8. Walisema mioyoni mwao,Na tuwaangamize kabisa;Mahali penye mikutano ya MunguWamepachoma moto katika nchi pia.