Zab. 73:21-25 Swahili Union Version (SUV)

21. Moyo wangu ulipoona uchungu,Viuno vyangu viliponichoma,

22. Nalikuwa kama mjinga, sijui neno;Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako.

23. Walakini mimi ni pamoja nawe daima,Umenishika mkono wa kuume.

24. Utaniongoza kwa shauri lako,Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.

25. Ni nani niliye naye mbinguni,Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.

Zab. 73