11. Nao husema, Mungu ajuaje?Yako maarifa kwake aliye juu?
12. Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki,Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi.
13. Hakika nimejisafisha moyo wangu bure,Nimenawa mikono yangu kwa kutokukosa.
14. Maana mchana kutwa nimepigwa,Na kuadhibiwa kila asubuhi.
15. Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo;Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako.
16. Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo;Ikawa taabu machoni pangu;
17. Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu,Nikautafakari mwisho wao.
18. Hakika Wewe huwaweka penye utelezi,Huwaangusha mpaka palipoharibika.
19. Namna gani wamekuwa ukiwa mara!Wametokomea na kutoweshwa kwa utisho.
20. Ee Bwana, kama ndoto wakati wa kuamka,Uondokapo utaidharau sanamu yao.
21. Moyo wangu ulipoona uchungu,Viuno vyangu viliponichoma,
22. Nalikuwa kama mjinga, sijui neno;Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako.