1. Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,Kwa hao walio safi mioyo yao.
2. Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka,Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza.
3. Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna,Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.
4. Maana hawana maumivu katika kufa kwao,Na mwili wao una nguvu.
5. Katika taabu ya watu hawamo,Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.
6. Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao,Jeuri huwavika kama nguo.
7. Macho yao hutokeza kwa kunenepa,Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao.
8. Hudhihaki, husimulia mabaya,Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu.
9. Wameweka kinywa chao mbinguni,Na ulimi wao hutanga-tanga duniani.
10. Kwa hiyo watu wake hugeuka huko,Na maji yaliyojaa humezwa nao.
11. Nao husema, Mungu ajuaje?Yako maarifa kwake aliye juu?
12. Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki,Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi.
13. Hakika nimejisafisha moyo wangu bure,Nimenawa mikono yangu kwa kutokukosa.