Zab. 72:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako,Na mwana wa mfalme haki yako.

2. Atawaamua watu wako kwa haki,Na watu wako walioonewa kwa hukumu.

3. Milima itawazalia watu amani,Na vilima navyo kwa haki.

4. Atawahukumu walioonewa wa watu,Atawaokoa wahitaji, atamseta mwenye kuonea.

5. Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua,Na wakati wa kung’aa mwezi kizazi hata kizazi.

6. Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa,Kama manyunyu yainyweshayo nchi.

7. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.

Zab. 72