2. Kwa haki yako uniponye, uniopoe,Unitegee sikio lako, uniokoe.
3. Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,Nitakakokwenda sikuzote.Umeamuru niokolewe,Ndiwe genge langu na ngome yangu.
4. Ee Mungu wangu, uniopoe mkononi mwa mkorofi,Katika mkono wake mwovu, mdhalimu,
5. Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU,Tumaini langu tokea ujana wangu.
6. Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa,Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,Ninakusifu Wewe daima.
7. Nimekuwa kitu cha ajabu kwa watu wengi,Na Wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.
8. Kinywa changu kitajazwa sifa zako,Na heshima yako mchana kutwa.
9. Usinitupe wakati wa uzee,Nguvu zangu zipungukapo usiniache.
10. Kwa maana adui zangu wananiamba,Nao wanaoniotea roho yangu hushauriana.
11. Wakisema, Mungu amemwacha,Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya.
12. Ee Mungu, usiwe mbali nami;Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia.
13. Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu.Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.
14. Nami nitatumaini daima,Nitazidi kuongeza sifa zake zote.