1. BWANA, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe,Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye.
2. Asije akaipapura nafsi yangu kama simba,Akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya.
3. BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya,Ikiwa mna uovu mikononi mwangu,
4. Ikiwa nimemlipa mabayaYeye aliyekaa kwangu salama;(Hasha! Nimemponya yeyeAliyekuwa mtesi wangu bila sababu;)
5. Basi adui na anifuatie,Na kuikamata nafsi yangu;Naam, aukanyage uzima wangu,Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.