29. Nami niliye maskini na mtu wa huzuni,Mungu, wokovu wako utaniinua.
30. Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,Nami nitamtukuza kwa shukrani.
31. Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng’ombe,Au ndama mwenye pembe na kwato.
32. Walioonewa watakapoona watafurahi;Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
33. Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji,Wala hawadharau wafungwa wake.